HOME

Feb 17, 2012

WAVAMIA NA KUIBA MAKUMBUSHO!!



Maafisa nchini Ugiriki wamesema kuwa wahalifu wa kutumia silaha wameiba kiasi kubwa cha sanaa za kale kutoka makumbusho ya taifa yaliyopo jiji la Ancient Olympia.


Meya wa jiji hilo Thymios Kotzias amekaririwa akisema kuwa wanaume wawili waliojifunika nyuso zao walivunja na kuingia ndani ya jengo hilo baada ya kumzidi nguvu mlinzi wa jengo hilo.


Waziri wa utamaduni wa Ugiriki Pavlos Geroulanos ameripotiwa kuwasilisha taarifa yake ya kujiuzuru ambapo makumbusho hayo yanaonekana kama moja ya sehemu muhimu ya kihistoria ya Ugiriki ambapo haijawekwa wazi ni kazi zipi za sanaa zilizoibwa ingawa ni nyingi.

No comments:

Post a Comment