HOME

Feb 23, 2012

HALI ILIVYOKUWA KATIKA MJI WA SONGEA..WAWILI WAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI!!






















Watu wawili wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi kufuatia vurugu zilizotokana na maandamano makubwa yaliyofanywa na wakazi wa mji wa Songea mkoani Ruvuma leo asubuhi kiasi cha kusababisha huduma za kijamii katika maeneo ya katikati ya mji kusimama kwa muda.


Wakazi hao wameandamana katika kile kinachodaiwa kuwa ni kushinikiza jeshi la polisi kuchukua hatua kudhibiti mauaji ya kiholela yanayoendelea mjini hapo kwa siku ya tatu mfululizo leo ambapo takribani watu sita wameuwawa katika matukio ya kutatanisha.

No comments:

Post a Comment