Youssou N’Dour |
Shirika la Umoja wa mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), limetangaza kuwa mwanamuziki mkongwe Youssou N’Dour, ameachia wadhifa wake kama balozi wa kujitolea katika shirika hilo.
Hatua hii inakuja kufuatia Youssou N’Dour, kuanza kwa kampeni zake za kuwania kiti cha uraisi wa Senegal, ikiwa ni nia yake aliyoitangaza siku chache zilizopita.
Kwa mujibu wa sera za UNICEF, wanasiasa ama mtu mwingine yoyote anayewania ofisi ya umma, hawezi kutumika kama balozi wa kujitolea wa shirika hilo.
No comments:
Post a Comment