HOME

Jan 10, 2012

MSANII ALPHA RWIRANGIRA AAMUA KURUDI SHULE!!

Alpha Rwirangira


Msanii kutoka nchini Rwanda, Alpha Rwirangira ameelekea nchini Marekani kuendeleza fani yake ya muziki katika chuo cha Campbellsville, kilichopo huko Kentucky.


Alpha ameondoka hivi karibuni, ambapo imefahamika kuwa amekwenda kusoma shahada ya muziki, katika kozi ambayo itachukua muda wa miaka mitano.


Mkali huyu wa muziki anayefahamika sana kwa wimbo wake wa Songa Mbele, ana matarajio ya kuzifanya ndoto zake katika muziki kutimia, pale atakapohitimu masomo yake huko Campbellsville.

No comments:

Post a Comment