HOME

Jan 9, 2012

UJENZI DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KARIBUNI!!

Dk. John Magufuli

Serikali ya Tanzania leo imetiliana saini na mbia mwenzake, shirika la hifadhi ya taifa (NSSF) ya ujenzi wa daraja la Kigamboni litakalogharimu shilingi bilioni 214.6 ambapo mradi huo unatarajia kuaanza muda wowote kuanzia sasa.


Daraja hilo hilo litajengwa na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group kwa kushirikiana na China Major Bridge Co Ltd za nchini China.

Waziri wa ujenzi, Dk. John Magufuli amesema ujenzi wa daraja hilo utaanza kabla ya mwisho wa mwezi huu, na utachukua miezi thelathini na sita kukamilika ambapo itakuwa mwezi januari 2015.

No comments:

Post a Comment