HOME

Jan 11, 2012

SERIKALI IMEREJESHA UTARATIBU WA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI!!

Mhe. Philipo mulugo
Wizara ya elimu na mafunzo ya  nchini Tanzania imetangaza kuendelea na utaratibu wa kuangalia kiwango cha wastani wa ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha pili ili kuendelea na madarasa yanayofuata ambapo kiwango hicho ni kile kinachofikia asilimia 30.


Akitangaza hatua hiyo naibu waziri wa elimu nchini Tanzania Mhe. Philipo mulugo amesema hatua hiyo inawapa nafasi wanafunzi wa kidato cha pili kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu mtihani huo tofauti na ilivyo sasa.


Mhe.Mulugo amesema pia wizara itapata nafasi ya kutathimi  maendeleo ya wanafunzi kabla ya mitihani ya kidato cha nne na kiwango cha ufundishaji kwa walimu katika shule za sekondari ambapo watakaofeli mtihani huo watarudia mara mbili katika kidato cha pili.

No comments:

Post a Comment