Floyd Mayweather na Manny Pacquiao |
Hapa wakitunishiana misuli |
Hatimaye bondia Floyd Mayweather ameupa ulimwengu wa ndondi kile hasa ulichokuwa ukikingoja - kutamka kwa maneno yake mwenyewe nia ya kizipiga na Manny Pacquiao
Hukumu yake ya kutumikia kifungo jela imesogezwa mbele hadi mwezi wa sita, kwa hiyo sasa anaweza kupanda ulingoni May 5 jijini Las Vegas.
Mashabiki wa ngumi kwa muda mrefu wamekuwa wakitamani kuwaona wanamsumbwi hao wakionyeshana ubabe ulingoni, na hatimaye sasa Floyd amejitokeza wazi na kumwambia Pacquiao naneno haya: "Ninakuita wewe, Manny Pacquiao, tupande ulingoni tupigane tarehe 5 mwezi wa 5, tuipe dunia kile inachotaka kukiona."
Floyd alikuwa akizungumza kwa kujiamini sana hasa katika mitandao ya Twitter na Facebook.
No comments:
Post a Comment