HOME

Jan 11, 2012

RIPOTI YAMSAFISHA RAIS KAGAME WA RWANDA!!

Rais wa Rwanda Paul Kagame

Hayati Juvenal Habyarimana.
Ripoti ya uchunguzi imeonekana kumfutia tuhuma Rais wa Rwanda Paul Kagame za kuchochea mauaji wa kimbari ya mwaka 1994 kwa kutungua ndege ya rais wa wakati huo Juvenal Habyarimana.


Wataalam wa uchunguzi  waliopewa jukumu na Ufaransa walitembelea eneo la tukio kutazama jinsi bomu lilivyorushwa na kutungua ndege hiyo.


Kutunguliwa kwa ndege hiyo ilikuwa moja ya vichocheo vilivyosababisha mauaji ya kimbari.


Uchunguzi wa awali wa Ufaransa ulimtupia lawama rais Kagame na washirika wake lakini ripoti ya sasa imesema Wahutu wenye itikadi kali ndio walimuua Habyarimana.

No comments:

Post a Comment