![]() |
Hayati Malam Bacai Sanha |
Kituo cha radio cha taifa huko Guinea-Bissau kimetangaza kuwa rais wa nchi hiyo Malam Bacai Sanha amefariki dunia akiwa hospitalini mjini Paris.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 64 aliyepata urais mwaka 2009 alisafiri kwenda Ufaransa kwa ajili ya kupata matibabu mwishoni mwa mwezi Novemba baada ya kupelekwa akiwa mahututi.
Haijawekwa hadharani maradhi yaliyokuwa yakimkabili ingawa ilikuwa ikijulikana kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.
Awali rais Sanha alikuwa akitibiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwenye hospitali ya nchi jirani ya Senegal ambapo amefariki dunia kwenye hospitali ya kijeshi ya Val de Grace kwenye mji mkuu wa Ufaransa.
No comments:
Post a Comment