![]() |
Gladys Koech |
Mwanamke mmoja anayesumbuliwa na matatizo ya kiakili kutoka nchini Kenya amewashangaza madaktari nchini humo baada ya kukukutwa na karibu dozen mbili za sindano ndani ya mwili wake.
Kwa mujibu wa gazeti moja la Kenya Vipimo vya kitabibu vya X-Ray vilivyofanywa kwa mgonjwa huyo Bi. Gladys Koech vilionyesha sindano zikiwa zimetapakaa katika sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwa ni pamoja na maeneo ya kifuani,miguu,mikononi pamoja na mgongoni.
Mume wa mwanamke huyo Bw. Philip Koech amesema mke wake aliumwa sana usiku wa kumkia sikukuu ya krismas desemba mwaka jana baada ya kulalamika kuhisi maumivu makali kutokana na kuvimba mguu hali iliyompelekea kushindwa kutembea.
No comments:
Post a Comment