HOME

Jan 9, 2012

IEBC KENYA YAZINDUA RIPOTI MPYA YA MAJIMBO MAPYA!!

Issack Hassan


Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC) leo imezindua ripoti ya awali ambayo inapendekeza uanzishwaji wa majimbo mapya ya uchaguzi na kupitia mipaka ya majimbo mengine.


Mwenyekiti wa IEBC Issack Hassan amezindua ripoti hiyo na kutoa wito wa kuvumiliana wakati wa mijadala ya wazi ambayo imepangwa kuanza kufanyika kuanzia kesho juu ya masuala yanayohusiana na uanzishwaji wa  majimbo mapya 80 ya uchaguzi.


Naibu waziri mkuu Musalia Mudavadi, ambaye alihudhuria uzinduzi huo ameitaka tume ya IEBC kuhakikisha kuwa kila sauti ya mijadala ya wazi inasikika na kuionya tume hiyo kuwa macho na mivutano ya kikabila ambayo inaweza kuibuka.

No comments:

Post a Comment