Mh. Shamsi Vuai Nahodha |
Idara ya uhamiaji nchini Tanzania imeendesha msako maalumu na kufanikiwa kukamata mtandao unaojishughulisha na biashara haramu ya binadamu unaoongozwa na mtu aitwaye Ashok Nepal raia Bangladesh.
Naibu kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo amesema kuwa katika operesheni hiyo jumla ya watu kumi na sita wamekamatwa wakiwemo raia kutoka nchi za Pakistani, Nepal na Kenya.
Kwa mujibu wa Bi. Hokororo, Ashok anatuhumiwa kuwaingiza chini isivyo halali watu hao na baadaye kuwatafutia viza kwenda nchini Afrika Kusini kwa malipo ya dola za Marekani elfu tano au dawa za kulevya zenye thamani hiyo hiyo ya fedha.
Mwishoni mwa mwaka jana waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Shamsi Vuai Nahodha aliitaka idara ya uhamiaji kujitathimini endapo inatimiza majukumu yake sawasawa baada ya kuwepo wimbi la wahamiaji haramu.
Katika maelezo yake waziri Nahodha alienda mbali na kuwataka maofisa wa uhamiaji kupima kama wanastahili kubaki na nyadhifa zao baada ya kuwepo tuhuma kwamba baadhi yao wamekuwa wakipokea rushwa na hivyo kufanikisha wahamiaji hao kuingia na kuishi nchini.
No comments:
Post a Comment