![]() |
Anwar Ibrahim |
![]() |
Anwar na mkewe |
Kiongozi wa upinzani nchini Malaysia, Anwar Ibrahim ameondolewa makosa ya ulawiti katika kesi iliyochukua karibu miaka miwili.
Jaji wa mahakama hiyo Mwanasiasa huyo alituhumiwa kufanya ngono na aliyekuwa msaidizi wake wa kiume.
Hata hivyo jaji wa mahakama hiyo Zabidin Mohamad Diah amesema uchunguzi wa DNA haukutoa ushahidi wowote.
Bw. Anwar mwenye miaka 64 amekanusha mashtaka yote akiyaita mpango wa kumchafua kisiasa ambapo serikali imesema nguvu ya mahakama nchini Malasyia iko huru na haina msukumo wa serikali.
Punde baada ya mahakama kutangaza uwamuzi huo, ndugu wa Bw Anwar walionekana kububujikwa na machozi ya furaha huku wafuasi wake wakishangilia uamuzi huo.
Wafuasi wa mwanasiasa huyo waliokusanyika nje ya mahakama mjini Kuala Lumpar wamekuwa wakisisitiza
kwamba kesi hiyo haikufaa kufunguliwa tangu kuwasilishwa kwa tuhuma za ulawiti.
No comments:
Post a Comment