Jan 10, 2012
KAMPUNI YA OPHIR ENERGY LEO IMETOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO!!
Kampuni ya Ophir Energy imetoa matenki 30 yenye ujazo wa lita 5000 kila moja na yenye thamani ya zaidi ya millioni 18 kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyolikumba Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka jana na sasa wanahamishiwa eneo la Mabwe pande, Bunju.
Msaada huo umekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Meck Sadiki katika eneo la Mabwepande ambapo mchakato wa kuwahamishia waathirika hao katika viwanja vilivyotolewa na serikali umeanza.
Msaada huu ni kufuatia mwito wa serikali kwa makampuni na watu binafsi kutoa missada ambayo itawasaidia waathirika katika makazi mapya huko Mabwepande.
Akitoa msaada huo, Meneja Uhusiano wa Masuala ya Serikali, Fidelis Lekule alisema ni matumaini yao kuwa msaada huo utatumika kama ilivyokusudiwa ili kuhakikisha kuna maji ya uhakika na pia kuhakikisha
mazingira ya familia zitakazohamishiwa Mabwepande ni safi.
“Tumetaarifiwa kuwa zaidi ya familia zitahamishiwa katika eneo hili kwa hiyo maji ya uhakika ni muhimu. Ni matumaini letu kuwa msaada huu utatumika vizuri ili familia hizi zipate huduma kwa muda mrefu zaidi,”
alisema.
Alisema: “Tunatoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na mali katika janga hili na sisi tuko tayari kuendelea kuisaidia serikali na jamii zinazokumbwa na matatizo mbalimbali.”
Alitoa wito kwa makampuni mengine na mashirika kutoa misaada mingine ilikuhakikisha familia hizi zinahamishiwa katika makazi mapya kwa muda unaotakiwa. “Tunatoa shukrani zetu kwa Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa
ujumla kwa kukubali kupokea msaada huu,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa alitoa pongezi kwa kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia waathirika hao wa mafuriko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment