Siku moja nilikuwa nabadilishana mawazo na vijana wenzangu kupitia email yangu,Je kwa siku wanachukua masaa mangapi kufikiri?lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza na kusema kuwa angalau kwa mwezi mmoja ana muda wa kukaa chini na kutafakari mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika maisha yao au kwa lugha nyingine mambo yanatokeo kwa lolote liwe tu(haphazardly),nilisikitika sana,nikawa najiuliza sasa je kama vijana wa sasa wengi tumekosa muda wa kutafakari angalau nusu saa kwa siku je tunajitakia nini katika maendeleo yetu sana sana ya kiuchumi ya sasa na ya muda mrefu na yale ya kijamii katika kuyatatua?ndugu msomaji fikiria tajiri dunia kama Bill Gates kwa muda mrefu namba moja duniani anatumia muda wa mwenzi mmoja kwenda kwenda katika kisiwa na kufikiri ni jins gani aendeleze biashara yake,nilisha wahi andika makala juu ya kutofikiri leo umempa mtu nafasi akufikirie na kisha kukutawala pasipo wewe kujua,ndugu yangu binadamu wote ni sawa ila tunafanyaje ili kuutimiza huu usawa?Ndugu ya asilimia 3% ya watu dunia wana malengo (plan) na wameyaandika ,asilimia 97% ya watu dunian hawana malengo maishani mwao kwa lolote tu lile likitokea nao humo humo yaani kwao kufanikiwa ni bahati,hii ni kutokana na kukosa muda wa kufikri ili wajikomboe,sababu hii inasabisha asilimia kubwa sana unaona duniani inatawaliwa na watu wachache sana,Askofu mkuu wa kanisa la Living faith dunian kutoka Nigeria anasema anatumia muda wake mwingi kufikiri kuliko kusoma biblia na vitabu vingine na kweli ni mmoja wa watu wenye mafanikio sana hapa kwetu Afrik kiuchumi,waafrika wengi wanapenda kufanikiwa lakini hawana hata sekunde moja ya kutafakari je tutafika?kuna mambo mbalimbali niliwahi kujifunza kwa wanazuoni mbalimbali mmoja wapo ni Dr John Maxwell katika kitabu chake cha “Thinking for Change”,kuna jinsi mbali mbali za kufikiri ambazo zina tija kama ukiwa makini:
1.kufikiri kwa zingatio moja(ondoa mambo mengine yote),uwezo wa kufikiri kwa kuondoa mambo yanayochanganya kwenye akili yako
2.Kufikiri kwa ubunifu,uwezo wa kuvunja sanduku la mipaka yako na kugundua mawazo mapya kabisa
3.kufikiri kimkakati,uwezo wa kutekeleza msisimuko wako na kutumaini kupata ufumbuzi kwa yasiyowezekana
4.kufukiri kwa uhalisi,uwezo wa kujenga msingi imara juu ya kuweza kufikiri kwa uhakika
5.kufikiri kiuwezekano,uwezo wa kuelekeza msisimuko wako na kutumaini kupata ufumbuzi kwa yasiyo wezekana
6.Kufikiri kwa kukosoa,uwezo wa kukataa mipaka ya wazo lililozoeleka ili kupata matokeo yasiyoya kawaida
7.kufikiri kwa pamoja,uwezo wa kuhusisha mawazo ya wengine ili kupata matokeo unganishi
8.kufikiri kusipo kwa ubinafsi,uwezo wa kuwafikiria wengine na safari yao ili kufanikisha ushirikiano
Mtu anayefikiri ana faida kubwa sana,kwanza hukoa muda mwingi wa ufanyaji jambo Fulani,kwa kuwa hutumia kanuni ya 20/80 huwa na kujiamini ya kutosha ambapo ni jambo la msingi,kuwavutia wengi jambo unalolifanya maana huku kurupuka.Ni raisi sana kuanza kufikiria anza sasa kupanga muda ambao kila siku utapenda kuwa peke yako na hali ya utulivu ukitafakari muda mzuri mara nyingi ni asubuhi alfajiri,usiku saa pale ambapo hakuna usufumbufu,
Ndugu yanguwatu wanasema mtu asiyekuwa na taarifa (habari)hana tofautina mnyama anayetembe barabarani lolotelile laweza kumtoke aendako kwa kuwa hana taarifa,mimi nasema ukiwa haufikirii ni kumpa tikeki mtu anayefikiria kukutawala,anza sasa kuweka ratibu ya kufikiri kwa siku sana sana usiku au asubuhi,ufanye moyo wako uwe unatamani kujua mengi mazuri,,kuna faida nyingi za kufikiri ikiwepo kuongeza thamani ya jambo unalolifanya napia kuwavutia watu jambo unalolifanya,anzan sasa anza leo.Maendeleo ya biashara zetu yanatokana na sisi tunavyofikiria,maendelo ya nchi tulionayo leo ni kutokana viongozi wetu walivyofikiria je walikuwa makini au walikopi kutoka kwa wengine? unaweza amua leo ukawa kati ya kundi dogo la watu duniani wanafikiria ili usitawaliwe na wengine na uwe na maendeleo maana blue print yako inatokana na wewe unajituma kufikiri.
WRITER:Deogratius kilawe ni mfanyabiashara hapa daresalaam,mshauri masuala ya biashara
0717109362au
email deogratiuskilawe@yahoo.com