HOME

Feb 3, 2012

BUNGE LIMEPINGA AZIMIO LA USHURU WA MAJI YA CHUPA KUPUNGUA!!

Waziri wa fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo bungeni mjini Dodoma























Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limekataa kuridhia azimio la marekebisho ya jedwali la nne la sheria ya ushuru wa bidhaa lililotaka kupunguza ushuru wa maji kutoka shilingi 69 kwa  lita moja hadi shilingi 12 kwa kuwa halina manufaa kwa mlaji wa kawaida.


Wakichangia azimio hilo baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Buchosa,mh. Charless Tizeba amedai punguzo hilo la ushuru linalenga kuwanufaisha wafanaybiashara wenye viwanda vya maji na halitaonekana kwa mwananchi wa kawaida, huku wabunge wakiitaka  serikali kuongeza ushuru wa bidhaa zinazotoka nje badala ya kushusha bidhaa za ndani


Akiwasilisha maoni ya kamati, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya fedha na uchumi mh. Abdalah Kigoda amesema kupunguzwa kwa ushuru bidhaa ya maji kutoka shilingi 69 hadi 12 kwa lita ni kutokana na ongezeko hilo kuathiri ushindani hasa katika bidhaa za ndani.

No comments:

Post a Comment