HOME

Feb 29, 2012

KAMPENI YA KUPUNGUZA UMRI WA URAIS HAINA UHUSIANO NA MIMI KUTAKA KUGOMBEA URAIS 2015!!


KABWE ZUBERI ZITTO, MP
KIGOMA KASKAZINI


   Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais’. Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais. Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama change, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.
    Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais. Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu. Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu. Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.
    Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.

Dar es Salaam


29 Februari 2012

Feb 28, 2012

SHAMBULIO LINGINE NIGERIA!!


Watu wenye silaha wamepanga mashambulzi na kulipua kituo cha polisi na benki iliyokuwa karibu Kaskazini mwa mji Nigeria katika mfulululizo wa mashambulizi mengine ya mabomu yanayodaiwa kufanywa na kundi la waislamu la Boko Haram kwa mujibu wa mashuhuda.


Shambulio hilo katika mji wa Jama'are kaskazini mwa jimbo la Bauchi limetokea saa 24 kabla ya kutokea tukio lingine la ukatili kama hilo katika mji mwingine kaskazini mwa Nigeria ambalo lilisababisha vifo vya askari polisi watatu.


Wakazi wamesema idadi kubwa ya watu wenye silaha walihusika na shambulio siku ya Jumatatu lakini hawakutaja idadi ya majeruhi.

SLEEPING PILLS 'LINKED TO INCREASED DEATH RISK'!!


Sleeping pills used by thousands of people in the UK appear to be linked with a higher death risk, doctors warn.


The American study in BMJ Open compared more than 10,000 patients on tablets like temazepam with 23,000 similar patients not taking these drugs.


Death risk among users was about four times higher, although the absolute risk was still relatively low.


Experts say while the findings highlight a potential risk, proof of harm is still lacking.

VETA YAPEWA CHANGAMOTO!!


Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ameitaka  Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) iwe chanzo cha kuibua ajira kwa kuwaandaa vijana hata walioko mbali kuwa wajasiriamali kwa kutumia mkongo wa mawasiliano.


Dk. Bilal ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi chuo cha VETA Makete akiwa katika  ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.


AMEsema hivi sasa dunia ipo katika ushindani  na mambo mengi yanakuwa kwa haraka zaidi na hivyo kuwataka waangalie uwezekano wa kutumia mkongo wa mawasiliano katika kukuza elimu ya ufundi kwa walio mbali  na wao wafaidike na elimu hiyo ili waweze kujiajiri.

GAVANA WA ZAMANI NIGERIA AKIRI MAKOSA!!

Bw. James Ibori

Aliyekua Gavana wa mojawapo wa majimbo yanayozalisha mafuta kwa wingi nchini Nigeria James Ibori, amekiri katika mahakama ya Uingereza ,mashataka kumi ya kuhusika na biashara haramu ya fedha na pia njama ya kughushi.


Polisi wa Uingereza wanamshtumu kwa kuiba takriban dolla $400m katika kipindi cha miaka 8.
Bw Ibori, ambae wakati mmoja alichukuliwa kua mmojawapo wa wanasiasa tajiri na mwenye ushawishi mkubwa alikamatwa mnamo mwaka 2007.


Baadae aliachiliwa ,kabla ya kukamatwa tena mjini Dubai kutokana na hati ya Uingereza na kusafirishwa hadi Uingereza.


Mnamo mwaka 2007, mahakama ya Uingereza ilipiga tanji mali zake zote zilizoshukiwa kuwa za thamani ya dolla millioni 35.


Mshahara wake kama gavana wa jimbo la Delta ulikua chini ya dola 25,000.

MREMA ATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU POSHO!!

Mbunge wa vunjo Dk. Augustine Mrema

Mbunge wa vunjo ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa nchini Tanzania, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema amesema hatojiuzulu wadhifa wa ubunge kwa kisingizio cha posho ndogo.


Mrema amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya vyombo vya habari kumnukuu spika wa bunge, Bi. Anna Makinda akisema kuwa takribani asilimia sabini ya wabunge wanataka kuacha ubunge kutokana na maslahi madogo wanayopata kama wabunge.


Kwa mujibu wa Bw. Mrema, yeye ameamua kuwatumikia Watanzania pasipo kuweka maslahi yake binafsi na kutolea mfano jinsi alivyothubutu kujiuzulu wadhifa wa uwaziri katikati ya miaka ya tisini kwa kile alichodai kuwa ni kutetea maslahi ya wanyonge.

MCHUANO MKALI UCHAGUZI SENEGAL!!

Rais Abdoulaye Wade akipiga kura yake

Mchuano mkali unaendelea katika uchaguzi wa Urais wenye utata nchini Snegal kati ya Rais wa sasa Abdoulaye Wade na waziri mkuu wa zamani Macky Sall.


Taarifa za awali kutoka Senegal ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha kuwa kuna mchuano mkali kati ya Rais wa sasa Abdoulaye Wade na waziri mkuu wa zamani Macky Sall na vyombo vya habari vya ndani na Bw Sall vinasema hakuna mgombea aliyefikia 50% inayotakiwa kuepuka duru ya pili.


Rais Wade, 85, anawania kwa awamu ya tatu nafasi hiyo licha ya kutumikia vipindi viwili vinavyoruhusiwa na katiba.


Bw. Wade alizomewa wakati alipokwenda kupiga kura Jumapili katika mji mkuu,Dakar.

Feb 27, 2012

ALLAN LUCKY ''RAIS WA WANAFUNZI'' NA HAIKA SAMWEL WAMEREMETA!!











                                                                                                                          ZAIDI:ZAMA HUMU

Feb 24, 2012

MWIGIZAJI DOTNATA AFANYIWA UPASUAJI!!

Husna Posh

Mtayarishaji na mwigizaji wa filamu Swahiliwood Husna Posh ‘Dotnata’ wiki iliyopita alifanyiwa upasuaji mkubwa kutokana na matatizo ya tumbo baada ya kuugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya THI iliyopo Kinondoni akiongea na FC nyumbani kwake Dotnata amesema kuwa anamshukru Mungu kwa kufanyiwa upasuaji mkubwa na kuamka salama na kuweza kuendelea na hali yake vema kwani tatizo lilikuwa kubwa.


“Namshukru kwanza Mungu wangu pili ni hawa Madaktari waliofanikisha zoezi hili na kunirudisha katika hali yangu ya kawaida, sasa naendelea vema kwa sasa muda mwingi nitatumia kwa mapumziko huku nikiendelea na matumizi ya dawa, lakini kwa sasa nipo safi kabisa na madaktari wangu ni mabingwa na walitoka nje kwa ajili ya kazi hiyo tu,”alisema Dotnata.
Husna Poshi


Kutokana na upasuaji huo Dotnata amesema kuwa anatakiwa kupumzika kwa muda wa miezi sita bila kufanya kazi yoyote nzito wala haruhusiwi kuendesha gari, kwa mantiki hiyo hata kuigiza atahitaji kuigiza zile sehemu zisozo na kurupushani kwa kufanya hivyo anaweza kupata matatizo. 

Chanzo:FilamuCentral

RAIA WATOROKA VITA MALI!!


Umoja wa mataifa umesema kuwa idadi ya watu wanaokimbia maeneo ya Kaskazini mwa taifa la Mali sasa imeongezeka na kufikia watu 20,000.


Takribani watu nusu milioni wamekimbilia mataifa jirani baada ya kundi jipya la waasi wa Tuareg kuanzisha mashambulio dhidi ya vikosi vya serikali wiki iliyopita.


Kwa mujibu wa umoja wa mataifa takriban watu 1000 wanavuka mpaka wa Mali na kuingia katika mataifa jirani kila siku.

DEVIL KINGDOM YAINGIA KATIKA FESTIVAL YA KIMATAIFA YA FOFA NCHINI GHANA!!


''
''Ndugu mashabiki wangu ile filamu yetu niliyomshirikisha Ramsey Nouah toka Nigeria ''Devil kingdom''imeingia katika tamasha la kimaifa la filamu nchini Ghana lijulikanalo kama Festival of films,Africa(FOFA) tamasha hili litaanza tarehe moja mwezi March hadi tarehe 4 March jijini Accrah-Ghana ambapo mastaa mbalimbali wa movie toka Africa na nje ya Africa watakuwepo,katika tamasha hili filamu nyingine toka Ghana,Nigeria,Africa kusini,Kenya,diaspora nk nazo zimeingia humo.mengi zaidi nitawajuza muda ukifika''.-STEVEN KANUMBA

MAPATO STARS VS DRC YATANGAZWA!!


Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) lililofanyika jana (Februari 23 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 32,229,000.


Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 11,420 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000 na sh. 15,000.


Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 5,916,288, gharama ya kuchapa tiketi sh. 2,250,000, malipo kwa kamishna wa mchezo sh. 150,000, malipo kwa waamuzi wanne sh. 480,000, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000.


Nyingine ni asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 3,676,542, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,838,271, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 919,136 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 11,948,763.

MZIGO MPYA WA P SQUARE NA AKON!!

NIPO NA NITAENDELEA KUWEPO THT - AMINI!!


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Jumba la vipaji Tanzania (THT), Amini Mwinyimkuu almaarufu kama Amini amekanusha uvumi uliopo mtaani na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini kuwa amefukuzwa katika Jumba hilo la vipaji (THT).


Akizungumza na Blog hii Amini ambaye ni mpenzi zilipendwa wa mwanamuziki Linah amesema ameshangazwa sana na uvumi huo wa kuwa yeye(Amini) amefukuzwa THT na kuongeza kuwa habari hizo hazina ukweli na ni uzushi mtupu.


Hata hivyo amesema anafikiri kuwa uzushi huo umetokana na ukimya wake wa kutotoa wimbo wowote kwa kipindi kirefu na kuongeza kuwa tayari amesharekodi wimbo wake mpya alioupa jina la ni wewe ambao anatarajia kuanza kuusambaza kwenye vituo mbalimbali vya Redio mapema wiki ijayo. 
ZAIDI:ZAMA HUMU

Feb 23, 2012

KAA TAYARI KWA UJIO MPYAA WA MUSA HUSSEIN!!

VYOMBO VYA HABARI KUANZA KUTUMIA MFUMO WA DIGITAL 2013!!

Waziri wa mawasiliano,sayansi na teknolojia, Prof. Makame Mbarawa

Vyombo vyote vya habari vinavyorusha matangazo yake kwa mfumo wa tekonolojia ya analojia nchini Tanzania, vimeagizwa kuwa ifikapo Disemba thelathini na moja mwaka huu, viwe vimezima mitambo yao na kuanza kurusha matangazo kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya digitali.


Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ametoa agizo hilo ambalo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika Mashariki wa kuhakikisha ifikapo mwaka 2013 matangazo yote ya radio na televisheni yawe yanapatyikana kwa mfumo wa teknolojia ya digitali.


Kwa mujibu wa Prof. Mnyaa, serikali inatambua athari yas gharama zitakazowakumba watumiaji wa huduma za matangazo ya radio na televisheni ambao watatakiwa kununua ving'amuzi na kwamba inafikiria uwezekano wa kuwataka waagizaji wa vifaa vya digitali kupunguza bei ya vifaa hivyo ili watu w asio na uwezo wamudu kuvinunua.

MTOTO WA GADDAFI ATAKA NYARAKA ZA KIFO CHA BABA YAKE!!


Mwanasheria wa mtoto wa kanali Muammar Gaddafi amefungua shauri kisheria katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu (ICC) kutaka nakala ya vyeti vya kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Libya.


Mwanasheria huyo wa Aisha Gaddafi, Nick Kaufman amesema hatua hiyo inachukuliwa kama sehemu ya kuonyesha kuwa baraza la serikali ya mpito ya Libya haikuendesha kwa usawa kesi ya kaka yake  Saif al-Islam ambaye alikamatwa jangwani kusini mwa nchi hiyo mwezi Novemba mwaka jana.


Mahakama hiyo ya makosa ya uhalifu huko The Hague,Uholanzi imemwambia mtoto huyo wa Gadafi,Aisha ambaye yupo nchini Algeria kutafuta taarifa kutoka kwa mamlaka mpya za Libya.


Hata hivyo mwanasheria  Kaufman amesema hakuna upande wowote wa serikali mpya uliokubali maombi yake ya kutaka taarifa juu ya kifo cha baba yake.

WATU 50 WAMEKUFA KATIKA SHAMBULIZI IRAQ!!


Takribani watu 50 wamekufa na wengine mamia kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu na risasi mjini Baghdad.


Maafisa wamesema kuwa mashambulizi hayo yanaonekana kuwalenga zaidi maafisa wa polisi ambapo watu tisa wameuwawa katika shambulizo baya zaidi katikati ya wilaya ya  Karrada ambapo wanaishi watu wa dhehebu la Shia.


Mlipuko karibu na kituo cha polisi umetingisha majengo na kuharibu maduka ambapo hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na mashambulizi hayo,Mashambulizi nchini Iraq yameibuka tangu kuondolewa kwa majeshi ya Marekani mwezi Desemba.

WAYNE ROONEY KUIKOSA MECHI DHIDI YA AJAX!!

Mshambuliaji Wayne Rooney

Mshambuliaji Wayne Rooney atakosa mchezo wa leo wa marudiano wa ligi ya Europa dhidi ya Ajax kutokana na kukabiliwa na maambukizi kwenye koo lake.


Rooney alikuwepo kwenye mazoezi hapo jana akiwa na wachezaji wenzake wa Manchester United, lakini alirejeshwa nyumbani kutokana na kuwa mgonjwa.


Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson, amesema anampumzisha mchezaji huyo, akiwa na matumaini ifikapo jumapili atakuwa fiti kwa mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Norwich.

SOMALIA URGED TO SEIZE ITS CHANCE!!

US Secretary of State Hillary Clinton

World leaders have urged Somalis to seize an "unprecedented opportunity" to rebuild their nation, at a gathering in London on the war-torn nation's future.


Ending threats of terrorism and piracy were in everyone's interests, UK Prime Minister David Cameron said.


Hillary Clinton said plans to elect leaders and adopt a constitution before August were "ambitious".


But she said the mandate of the UN-backed interim government would not be extended any longer.


Somalia has endured more than two decades of civil war and famine.

SERIKALI YASHINDA KESI YA ''SAMAKI WA MAGUFULI''!!




Mahakama kuu ya Tanzania ,leo imetoa hukumu dhidi ya raia wa tano wa China wanaokabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika ukanda wa Tanzania kwa kutumia meli ya Tawariq 1 maarufu kama ‘Kesi ya Samaki wa Magufuli’.


Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Agustine Mwarija imeamua washtakiwa wawili kati ya watano ambao ni Hsu Chin Tai, Zhao Hanguing wamekutwa na hatia ya kufanya uvuvi katika ukanda wa bahari ya Hindi na kuhukumiwa faini ya shilingi bilioni moja au kifungo cha miaka 20 jela kwa wote wawili lakini Zhao Hanguing alikutwa na kosa jingine hivyo alitakiwa kulipa faini ya shilingi bilioni 20 au kifungo cha miaka 10 ambapo upande wa mashtaka umeiomba mahakama itaifishe meli waliyokuwa na na jaji akakubali na sasa ni mali ya serikali.


Wengine Hsu Shang Pao, Ca’ Dong Li na Chen Rui Hai wameachiwa huru ambapo Mwarija amesema washtakiwa hao wanaweza kukata rufaa kwani milango iko wazi.


Machi 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakama Kuu wakikabiliwa na makosa ya kuvua samaki bila leseni, kuharibu mazingira katika kina kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

WABUNGE KENYA WAOMBOLEZA KIFO CHA WAZIRI WA MAZINGIRA!!


Wabunge wa bunge la Kenya jana wameahirisha shughuli za bunge mara mbili kuomboleza kifo cha waziri wa mazingira  John Michuki ambaye amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo Jumanne usiku.


Bunge hilo kwa mara ya kwanza liliahirisha shughuli zake asubuhi na mchana wakati wabunge walipokuwa wakimzungumzia Bw. Michuki kama kiongozi mkweli na shujaa wa taifa hilo.


Rais Kibaki jana aliagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo ambapo baadae jioni makamu wa rais Kalonzo Musyoka,spika wa bunge  Kenneth Marende na wabunge kadhaa waliitembelea familia ya Bw. Michuki huko Ridgeways jijini Nairobi.

SOMALIA KUJADILIWA LONDON!!


Tishio la ugaidi na uharamia ni miongoni mwa masuala yatakayo jadiliwa katika mkutano huo wa London kuhusu hatma ya Somalia.


Wawakilishi kutoka nchi 40 watahudhuria mkutano huo wenye lengo la kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba nchi hiyo kufuatia miongo miwili ya vita na ukame.


Viongozi wanatarajiwa kukubaliana kuhusu pesa za ujenzi wa shule, hospitali na idara ya polisi.


Uingereza imeielezea Somalia kama nchi iliyoporomoka zaidi duniani lakini imesema kuna haja ya kuipa Somalia nafasi nyingine ili iweze kuibuka kutoka matatizo yake.


Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali, ambaye ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano huo ameonya kuwa nchi yake iko katika njia panda na inahitaji usaidizi mkubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa.

TEVEZ AOMBA RADHI MAN CITY!!


Carlos Tevez, mshambulizi wa Manchester City, ameomba radhi kwa tabia yake isiyofaa hivi majuzi, na iliyoanza tangu alipogombana na meneja Roberto Mancini mwezi Septemba.


Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 28, alirudi katika klabu ya Man City wiki iliyopita, baada ya kuchukua hatua mikononi mwake, alipoamua kurudi nchini Argentina kwa kipindi cha miezi mitatu.


Wakati huohuo Tevez amefutilia mbali malalamiko aliyokuwa amewasilisha rasmi dhidi ya klabu ya Man City.


Baada ya kushindwa kujiunga na AC Milan ya Italia kama ilivyotazamiwa wakati wa usajili wa mwezi Januari, Tevez bila shaka alikuwa na uamuzi mgumu wa kuamua iwapo aendelee kupumzika na akicheza golf huko Argentina, ama arudi tena mjini Manchester na kujaribu kupigania nafasi yake katika timu yake.

PRESIDENT KIKWETE MEETS UK'S FOREIGN MINISTER WILLIAM HAGUE IN LONDON!!

President Jakaya Mrisho Kikwete chats  with UK’s  Secretary of State for
Foreign and Commonwealth Affairs of the Mr William Hague and
thebParliamentary Under Secretary responsible for Africa, United Nations,
economic issues, conflict resolution, and climate change Mr Henry
Bellingham after their talks at the Foreign office  in London today
February 22, 2012.  The UK will host a conference on Somalia tomorrow
February 23, 2012 with the view to  pulling  together international effort
to help Somalia to its feet after 20 years of sliding backwards, despite
the efforts of the African Union, the United Nations and the international
community, international policy towards the country.

WAANDISHI WA HABARI WAWILI WAUWAWA SYRIA!!

Mwandishi Marie Colvin na mpiga picha Remi Ochlik

Serikali ya Ufaransa imethibitisha kwamba waandishi habari wawili wa kimataifa wameuawa katika mji wa Homs, Syria.


Msemaji wa serikali amesema waliokufa ni pamoja na Marie Colvin mwandishi wa kimataifa kutoka Marekani pamoja na mpiga picha raia wa Ufaransa Remi Ochlik. Bi Colin alikuwa mwandishi wa gazeti la Sunday Times huko Marekani.


Wanaharakati wa Syria wamesema wawili hao walikufa baada ya kombora kupiga nyumba walimokuwa wakipeperushia matangazo yao eneo la Baba Amr.


Kwenye ripoti yake hapo Jumanne Colvin alisema mashambulizi ya jeshi la serikali yalifanywa bila kujali usalama wa raia.


Mwanaharakati wa Syria ambaye amekuwa akitoa kanda za video pia aliuawa mjini Homs.

HALI ILIVYOKUWA KATIKA MJI WA SONGEA..WAWILI WAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI!!






















Watu wawili wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi kufuatia vurugu zilizotokana na maandamano makubwa yaliyofanywa na wakazi wa mji wa Songea mkoani Ruvuma leo asubuhi kiasi cha kusababisha huduma za kijamii katika maeneo ya katikati ya mji kusimama kwa muda.


Wakazi hao wameandamana katika kile kinachodaiwa kuwa ni kushinikiza jeshi la polisi kuchukua hatua kudhibiti mauaji ya kiholela yanayoendelea mjini hapo kwa siku ya tatu mfululizo leo ambapo takribani watu sita wameuwawa katika matukio ya kutatanisha.

Feb 21, 2012

NIKO IMARA KAMA MBUYU - RAIS MUGABE!!


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepuuza hofu kuhusu afya yake na kujigamba kuwa yuko imara kama mbuyu huku akiadhimisha umri wa miaka 88 leo.


Akihojiwa na radio inayomilikiwa na serikali jana rais Mugabe amesema iko siku ataugua lakini kwa sasa ni mzima alikaririwa akisema kiongozi huyo ambaye mtawala mwenye umuri mkubwa barani Afrika.


Mugabe ambaye ameliongoza taifa hilo tangu mwaka 1980 nchi hiyo ilipopata uhuru mara kadhaa amekuwa akikanusha kuwa mgonjwa amekuwa akisafiri kwenda nchini Singapore mara kwa mara mwaka huu na msemaji wake akisema kuwa rais alienda kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho,huku vyombo vya habari vikiripoti kuwa anasumbuliwa na saratani.

WATANZANIA KUNUFAIKA NA MADINI!!


Makampuni yanayowekeza katika sekta za nishati na madini nchini Tanzania yametakiwa kuzingatia umuhimu wa kutumia sehemu ya mapato yanayotokana na madini katika kuendeleza jamii za sehemu wanakofanya shughuli za utafutaji madini na nishati.


Waziri wa nishati na madini, William Ngeleja amesema hayo jijini Dar es Salaam leo muda mfupi baada ya kusaini mikataba miwili na kampuni ya Swala Limited ya kutafuta mafuta na gesi katika wlaya za Kilosa na Kilombero mkoani Morogoro na bondfe la Pangani mkoani Tanga.


Kauli ya waziri Ngeleja imefuatia ahadi iliyotolewa na kampuni hiyo ya kugawa bure sehemu ya hisa zake kwa wananchi wazawa wa maeneo husika kama njia ya kuwafanya wanufaike na rasilimali za madini yaliyo katika eneo yao.-

HAYE,CHISORA KUKABILIWA NA KIFUNGO!!

David Haye

Mabondia wa Uingereza David Haye na Dereck Chisora wanatuhumiwa kutenda makosa ya uhalifu ambayo adhabu yake ni kifungo baada kupigana hadharani huko Munich.


Waendesha mashtaka wa Ugerumani wameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kuwa bondia Haye anatuhumiwa kusababisha maumivu ya mwili ambalo ni kosa la jinai na ikiwa atatiwa hatiani adhabu yake ni miezi sita mpaka miaka kumi jela.


Chisora ambaye amekubali kuwa kitendo alichofanya hakikubaliki anatuhumiwa kujeruhi ikiwa ni pamoja na kutoa lugha ya vitisho kosa hilo adhabu yake ni miaka mitano jela.

AHAKAMA KUU YAKUBALI TANESCO KUIPINGA DOWANS!!


Mahakama Kuu Dar es Salaam imerejesha matumaini kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya kutupilia mbali pingamizi la Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans dhidi ya maombi yake ya kibali cha kukata rufaa.


Tanesco iliwasilisha maombi mahakamani hapo kutaka kibali cha kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya mahakama hiyo iliyoamuru kusajiliwa kwa tuzo ya Dowans ya Sh94 bilioni, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).


Hata hivyo, Dowans nayo kupitia kwa wakili wake, Kennedy Fungamtama iliweka pingamizi dhidi ya Tanesco ikiiomba mahakama hiyo iinyime kibali hicho cha kukata rufaa kwa madai kuwa haina haki ya kisheria kupinga hukumu hiyo.


ZAIDI:INGIA HUMU

Feb 20, 2012

WANAUME KENYA WAGOMA KULA MAJUMBANI MWAO!!

Mwenyekiti wa Chama cha maendeleo ya Kina baba Nderitu Njoka


















Waume nchini Kenya wanapanga kugomea vyakula vya mabibi zao kwa siku sita kutoka na kuongezeka kwa visa vya wanawake kuwapiga mabwana zao.


Badala yake wanaume watakuwa wakila mahotelini na magengeni


 amesema mgomo huo wa siku sita una lengo la kuwashinikiza wanawake kukoma kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.


Kiongozi huyo Nderitu Njoka amesema kuanzia leo jumatatu ataanza kampeni ya kuwashawishi akinababa kula mahotelini badala ya majumbani mwao.

MAUAJI YA KUTISHA YAKITHIRI MKOANI RUVUMA!!

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda

Kasi ya mauaji ya kutisha yanayotokea katika mji wa Songea mkoani Ruvuma inazidi kuongezeka kufuatia mtu mmoja kuuawa usiku wa kuamkia leo mwaka huu katika eneo la Lizaboni mjini Songea ambapo mwili wake ulikutwa ukiwa umekatwa katwa kwa kutumia mapanga.


 Kwa mujibu wa mashuhuda wa awali waliokuta mwili wa marehu huyo aliyejulikana kwa jina la Bakari Ally(20)  mkazi wa Lizaboni walisema kuwa alikuwa na muda wa miezi minne tangu afike hapo akitokea Tunduru na kupata kazi katika mashine ya kusaga nafaka ambayo alikuwa akiifanya mpaka mauti hayo yalipomkuta.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Februari 20 mwaka huu ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu aliuawa kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo kichwani.

IRAN YAACHA KUUZA MAFUTA ULAYA!!

















Wizara ya mafuta ya Iran inasema kuwa imeacha kuziuzia mafuta Ufaransa na Uingereza, kulipiza vikwazo vilivowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya mafuta ya Iran kuanzia mwezi wa Julai.


Msemaji wa wizara hiyo, alisema Iran badala yake itauza mafuta yake kwa wateja wepya.


Mapema mwezi huu, Waziri wa Mafuta wa Iran, alisema mafuta yataacha kupelekwa nchi za Ulaya, kabla ya vikwazo kuanza, lakini hakuzitaja nchi gani zitalengwa.


Umoja wa Ulaya na Marekani hivi karibuni ziliweka vikwazo vikali vipya dhidi ya Iran, na kuishutumu kuwa inatengeneza silaha za nuklia, kisirisiri.

BONDIA DERECK CHISORA AACHIWA HURU!!


Bondia Dereck Chisora ameachiwa huru bila ya kufunguliwa jalada la kesi Jijini  Munich, baada ya kupigana ngumi kavu kavu na bondia mwenzake wa Uingereza David Haye.


Haye na Chisora walipigana katika mkutano wao na waandishi wa habari, wa kutangaza pambano lao.  Polisi bado wanamtafuta Haye ambaye hajulikani alipojificha, kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.


Akizungumzia tukio hilo bondia anayeshikilia mkanda wa WBC, Wladimir Klitschko amesema ugomvi huo umeharibu heshima ya mchezo wa ngumi, na amemtaka Chisora na Haye waadhibiwe.

I AM AN EXPERT IN GOVERNANCE-MUSEVENI


President Yoweri Museveni has defended his long stay in power saying that it has helped him to learn many things and he is now an expert in governance.


The President who was the chief guest at the launching of the Great Lakes University of Kisumu Education Trust Fund told his audience that many African problems are a result of lack of proper research and wrong advice from outsiders.


He gave the example of power shortages in Uganda which have adversely affected the economy.


Museveni said that he had identified the problem in 1986 when he took over power that Uganda needed to construct its own dams to produce enough cheap power for its growing economy.

Source:New Vision Uganda

MWIMBAJI MAARUFU SUDAN AFARIKI DUNIA!!

Maelfu ya wananchi Sudan wakiwa wamebaba mwili wake

Mwimbaji maarufu wa Sudan, Mohammed Osman Wardi, amefariki mjini Khartoum akiwa na umri wa miaka 80.


Alivutia watu kupenda ala za asili za kabila lake, la WaNubi.


Kwa sababu ya maoni yake ya mrengo wa kushoto, Mohammed Osman Wardi alifungwa na Rais Jaafar Numeri katika miaka ya '80, na akahamia uhamishoni wakati rais wa sasa, Omar al-Bashir, aliponyakua madaraka mwaka wa 1989.

Feb 18, 2012

MAMA NA MTOTO WA WHITNEY HOUSTON WAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUELEKEA MAZISHI YA NYOTA HUYO WA MUZIKI DUNIANI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO!!





Mtoto wa Whitney Bobbi Kristina akiwasili msibani huko Whigham Funeral Home, New Jersey akiwa na majonzi makubwa


Mtayarishaji wa muziki ambaye pia alikuwa rafiki wa karibu wa mwanamuziki huyo Clive Davis alionekana akiwasili kwenye nyumba ya msiba akiwa ameongozana na mama Whitney Cissy na mtoto wake Bobbi Kristina

Aliyewahi kuwa mpenzi wa Whitney Houston Ray J akiwa ameongozana na dada yake Brandy kuelekea kwenye msiba wa mwanamuziki huyo

Waombolezaji wakiwa wamejipanga katika eneo hilo wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho