HOME

Apr 17, 2012

WESLEY KORIR NA SHARON CHEROP WANYAKUA UBINGWA BOSTON MARATHON!!

Mwanariadha wa Kenya Wesley Korir na Sharon Cherop wamenyakua ubingwa wa 116 wa Boston Marathon jana katika mpambano ambao ulikuwa na joto kubwa na kusababisha kasi kwa wanariadha ambao walitumia michuano hiyo kuwavutia makocha wanaochagua timu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki.

Korir alishinda kwa kasi ndogo ya kwa upande wa wanaume kwa kukimbia kwa muda wa masaa mawili dakika 12 na sekunde 40 na kumbwaka mkenya mwenzake  Levy Matebo ikiwa imesalia maili moja.

Matebo alishika nafasi ya pili kwa kukimbia kwa muda wa masaa mawili dakika 13 na sekunde 06, sekunde saba mbele ya  mkenya mwingine Bernard Kipyego aliyeshika nafasi ya tatu.

No comments:

Post a Comment