Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimetoa pole kutokana na kifo cha msanii mahiri nchini, Steven Kanumba kilichotokea mwishoni mwa wiki.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, ilieleza kuwa chama hicho kinaungana na wasanii wote nchini na Watanzania kwa ujumla kuombeleza kifo cha Kanumba.
“TASWA imeshtushwa na taarifa za kifo cha Kanumba, hivyo tunatoa pole kwa familia ya msanii huyo na wasanii wote wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na msanii huyo.
“Kanumba atakumbukwa na waandishi wa habari za michezo na burudani kutokana na ukaribu wake kwao na alikuwa na ushirikiano wa kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo, hali ambayo waandishi wa habari za michezo na burudani nchini wataendelea kumkumbuka.Mungu amuweke mahali pema peponi,” alisema Mhando.
No comments:
Post a Comment