HOME

Apr 26, 2012

TAHADHARI YA MAFURIKO YATOLEWA KENYA!!

Serikali ya Kenya imeonya wakazi wake wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja ili kujiepusha na mafuriko.


Katibu mkuu wa wizara ya programu maalum nchini Kenya  Bw. Andrew Mondoh ametoa taarifa ya tahadhari kwa maeneo ya Budalangi, Kano, Wareng Pokot, Baringo , Pwani na baadhi ya maeneo ya Nairobi kuwa maeneo makuu yanayoweza kuathiriwa na mafuriko katika siku sita zijazo.


Tahadhari hiyo inakuja kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zilizosababisha mafuriko katika maeneo kadhaa ambapo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu 36 na kuharibu mali.

No comments:

Post a Comment