Kiongozi mpiganaji wa demkrasia nchini Burma Aung San Suu Kyi anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Norway baada ya kipindi cha miaka 24.
Wizara ya mambo ya nchi za nje nchini Norway imeliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kuwa Aung San Suu Kyi anatarajia kufanya ziara nchini humo mwezi June.
Pia msemaji wa chama cha siasa cha kiongozi huyo ameliambia shirika la utangazaji la Reuters kuwa atafanya ziara nchini Uingereza kufuaTia mwaliko wa waziri mkuu David Cameron .
No comments:
Post a Comment