Viongozi wa nchi za Afrika magharibi ECOWAS wamekubaliana kupeleka majeshi nchini Mali na Guinea-Bissau kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika nchi hizo.
Umoja huo wa nchi za Afrika magharibi umesema kwamba baada ya mkutano wa dharura,viongozi hao wanatarajia kuona uchaguzi wa urais katika nchi hizo unafanyika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Kati ya askari 500 na 600 watapelekwa nchini Guinea-Bissau haraka iwezekanavyo wakati askari 3,000 kutoka umoja huo wanatarajiwa kupelekwa nchini Mali kusaidia majeshi ya nchi hiyo kupambana na waasi ambao wanadhibiti eneo la kaskazini.
No comments:
Post a Comment