HOME

Apr 4, 2012

WATU SABA WAMEKUFA KATIKA MLIPUKO NCHINI SOMALIA!!

Watu saba wamekufa mapema leo kufuatia mlipuko mkubwa katika ukumbi mpya wa kitaifa uliofunguliwa hivi karibuni uliopo jijini Mogadishu nchini Somalia.


Mlipuko huo umetokea wakati wa hafla ya kuamdhimisha mwaka mmoja tangu televisheni ya taifa kuanza kuyapeperusha matangazo yake.


Takriban watu saba wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, wakiwemo wabunge ambapo Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali alikuwepo kwenye hafla hiyo lakini haijabainika ikiwa alijeruhiwa.


Mshambuliaji wa kike wa kujitoa mhanga ameripotiwa kufanya shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment