HOME

Apr 18, 2012

SUDAN YA KUSINI NA KASKAZINI ZAIBUA WASIWASI!!

Sudan Sudan Kusini zimeshutumiana kwa kufungua eneo jipya la mpaka wa mapigano katika eneo linalogombewa na kuongeza wasiwasi wa kuzuka vita.


Mapigano yalianza kaskazini mwa Aweil Sudan Kusini kiasi cha maili 100 (160 kilometa) magharibi mwa Heglig eneo lenye mafuta, chanzo cha mapigano ya sasa.


Msemaji wa jeshi la Sudan amesema askari saba wa Sudan Kusini na raia 15 waliuawa.


Sudan Kusini ilijitenga mwaka jana lakini mpaka wake na Jamhuri ya Sudan haujafikiwa makubaliano.

No comments:

Post a Comment