Maelfu ya watu nchini Misri wanafanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Cairo kupinga uamuzi wa mkuu wa upelelezi wa rais Hosni Mubarak kusimama katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
Maandamano hayo katika uwanja wa Tahrir Square katikati ya jiji la Cairo yameitishwa na waislamu wenye msimamo mkali wa kundi la Muslim Brotherhood.
Waandamanaji hao wanasema kuogombea urais kwa Bw. Omar Suleiman ni jaribio la baadhi ya wanachama wa utawala wa zamanai rais wa zamani wa nchi hiyo Mubarak kurejea madarakani.
No comments:
Post a Comment