Majeshi Sudan Kusini. |
Rais Obama ametoa wito kuwa mapigano baina ya Sudan Kaskazini na Kusini yamalizwe, na marais wa nchi zote mbili wawe na ujasiri wa kutatua tofauti zao kwa amani.
Rais Obama amesema Sudan Kaskazini inafaa kusitisha hatua za kijeshi dhidi ya jirani yake pamoja na mashambulio ya ndege; na Sudan Kusini iache kusaidia makundi yenye silaha ndani ya Sudan Kaskazini, na harakati zake za kijeshi mpakani.
Baada ya Sudan Kusini kuviteka visima vya mafuta kwenye eneo la Heglig la mpakani siku kumi zilizopita, nchi hizo zilikaribia vita, lakini majeshi yake yameondoka, baada ya malalamiko ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment