HOME

Apr 24, 2012

HUKUMU YA TAYLOR KUTOLEWA ALHAMIS!!

Aliyewahi kuwa rais wa Liberia Charles Taylor
Hukumu ya aliyewahi kuwa rais wa Liberia Charles Taylor inatarajiwa kutolewa siku ya Alhamisi kufuatia mashitaka yanayomkabili ya kuwapa silaha waasi wa Sierra Leone ili apate madini ya almasi katika miaka ya 90.


Jopo la majaji watatu linatarajiwa kusoma hukumu hiyo ya kihistoria, ambayo ni ya kwanza dhidi ya kiongozi wa zamani wa nchi kuwahi kutolewa na mahakama ya kimataifa, katika mahakama maalum kuhusu Sierra Leone mjini Leidschendam nje ya The Hague.


Taylor mwenye umri wa miaka 64, anatuhumiwa kwa kuwasaidia waasi wa kundi la Revolutionary United Front – RUF la Sierra Leone, kufanya mashambulizi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya watu 120,000 kati ya mwaka wa 1991 na 2001.


Katika kesi hiyo iliyokamilika mwezi Machi 2011, mwanamitindo maarifu duniani Naomi Campbell alitoa ushahidi jinsi alivyopokea almasi kutoka kwa Taylor.

No comments:

Post a Comment