Hatimae zoezi la kuwaapisha wabunge wapya wa CHADEMA limefanyika leo Bungeni mjini Dodoma huku serikali ikisisitiza kuwa itaendelea kutoa huduma kwa wananchi wake bila kujali itikadi ya vyama vyao wala chama kinachoongoza eneo husika.
Zoezi hilo la kuapishwa kwa wabunge hao limefanyika huku kauli mbiu ya Peoples Power ikitawala jengo la bunge na kulazimika mafundi mitambo kuzima kwa muda mitambo ya sauti jambo ambalo halikuzuia tendo hilo kufanyika ambapo
mbunge wa v iti maalum CHADEMA Mh Cecilia Daniel Pareso ndiye aliyeanza kula kiapo na kufuatiwa na mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Samweli Nassari
Nje ya bunge mara baada ya wabunge hao kuapishwa walipongezwa na ndugu pamoja na jamaa walioambatana nao huku wakielezea kile ambacho wananchi wanakitarajia kutoka kwao
No comments:
Post a Comment