Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameshutumu mashambulio ya angani yanayofanywa na Sudan katika mipaka ya Sudan Kusini, na akiwataka viongozi wa nchi hizo mbili kuwacha kujiingiza katika vita.
Bw. Moon ameitaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.
Siku ya Jumatatu ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa
Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa kwa raia wa kawaida na hasara kubwa katika mji huo.
Awali, Rais wa Bw. Sudan Omar al-Bashir alipuuza uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment