Jeshi la polisi nchini Uganda limeanzisha upelelezi wa ndani ya jeshi hilo kwa maafisa wake ambao walihusika na tukio la kumkamata kiongozi wa wanawake wa chama cha FDC Ingrid Turinawe Ijumaa iliyopita kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.
Kiongozi huyo amedaiwa kufinywa matiti yake na kuwekwa wazi na maafisa wa polisi ambao walimtia mikononi wakati akielekea katika mkutano wa vyama vya upinzani huko Nansana.
Kundi la wanawake nchini Uganda wamevua nguo na kubaki vifua wazi wakilalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kijinsia mwanasiasa wa upinzani Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.
Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment