HOME

Apr 16, 2012

KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2012 (KTMA)!!

Luiza Mbutu akipokea tuzo ya Wimbo bora wa kiswahili wa bendi ni Dunia daraja wa African Stars iliyotolewa na Shamim Mwasha na Komandoo Hamza Kalala
TMK Wanaume wakitoa burudani usiku wa Jumamosi katika tuzo za Kili Music Awards
Kutoka kulia msanii Amini,Chaz Baba na Barnaba wakitoa burudani kama kundi la Sikinde kwa usiku huo.
Kutoka kushoto Ommy Dimpoz ''Kwa Pooz kwa pooz'',Diamond na Khalid Chokoraa wakitoa burudani kama Msongo Ngoma.
Wakali wa Comedy Tanzania King Majuto na Sharo Milionea wakiwa jukwaani tayari kutoa tuzo.
Baada ya miaka 12 ya kushiriki katika tuzo za Kili Music Awards Hatimaye Wimbo bora wa Taarabu Full Stop wa Khadija Kopa ulichukua tuzo hapo akiwa na mume wake na watoto wake waliokwenda kumpa support.
Msanii bora wa hiphop ni Roma akiwa amesindikizwa na rafiki yake Izzo Bussiness'' Izzo Biashara'' kupokea tuzo yake ya pili.
Recho anayetamba na kibao Kizunguzungu akitoa burudani
Mtangazaji wa kipindi cha Mseto East Africa Mzazi Willy Tuva akipokea tuzo ya Wimbo bora wa Afrika mashariki Kigeugeu kwa niaba ya Jaguar.
Rapa bora wa mwaka wa bendi ni Kalidjo Kitokololo aliondoka na yake moja.
Wimbo bora wa kushirikiana Nai Nai wa Ommy Dimpoz ft Ali Kiba hapo wakiwa jukwaani kutoa shukrani zao
Msanii bora anaechipukia Ommy Dimpoz akichukua tuzo yake ya pili akiwa na rafiki yake wa karibu Diamond.
Dayna akiperfom wimbo wa Saida Karoli.

No comments:

Post a Comment