HOME

Apr 11, 2012

TISHIO LA TSUNAMI BAHARI YA HINDI!!

Tetemeko la ardhi la Magnitude 8.7 limetikisa chini ya bahari katika jimbo la Kaskazini mwa Indonesia Aceh ambalo limetoa tishio ya kutokea Tsunami katika ukanda wa bahari ya Hindi.


Kituo cha Pacific Tsunami Warning(PTWC) kimesema bado haijajulikana iwapo Tsunami ianweza kutokea lakini kimezitaka mamlaka husika kuchukua tahadhari mapema.


Ukanda huo umekuwa ukikumbwa na matetemeko ya ardhi ambapo Tsunami katika bahari ya Hindi iliyotokea mwaka 2004 iliua watu elfu 170,000 huko Aceh.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imethibitisha kwamba leo huko Sumatra Indonesia kumetokea tetemeko maarufu kama Tsunami chini ya bahari ambapo hii hali inatarajiwa kutengeneza mawimbi ya Tsunami ambayo yanatarajiwa kufika kwenye pwani ya Tanzania  hasahasa sehemu za Mtwara kuanzia saa 11 jioni leo.

No comments:

Post a Comment