Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa takribani watu 38 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia mabomu mawili ya kutegwa ndani ya gari katika mji wa kaskazini wa Kaduna nchini kulipuka.
Watu wengi wamejeruhiwa wakati wa mlipuko huo uliotokea wakati maafisa waliposimamisha gari hilo wakati likitaka kuingia kanisani ambapo saa chache baadae bomu lililipuka katika mji mkuu wa Jos na kujeruhi watu kadhaa.
Hakuna kikundi au mtu aliyejitokeza kudai kufanya mashambulizi hayo lakini shutuma zinaelekezwa kwa kundi la Boko Haram kundi la kiislamu na kuonya kufanya mashambulizi siku ya Pasaka.
No comments:
Post a Comment