HOME

Apr 13, 2012

RIPOTI YABAINI UBADHIRIFU WA KUTISHA SERIKALINI!!

Kushoto ni mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Uttoh (picha maktaba)
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania (CAG) Ludovick Uttoh amewasilisha ripoti yake bungeni inayoonyesha kuendelea kuwepo kwa ufisadi wa kutisha serikalini, huku deni la taifa likiongezeka kutoka shilingi Trilioni 10.5 mwaka juzi na kufikia shilingi trilioni 14.4 mwaka jana.


CAG amesema serikali imetumia shilingi bilioni 544 bila ya kuidhinishwa na bunge, shilingi bilioni 1 zimelipwa mishahara kwa watumishi hewa na shilingi bilioni 3 zimetumika katika balozi za Tanzania nje ya nchi ambazo zipo nje ya bajeti iliyoidhinishwa na bunge.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG pia amesema baadhi ya mashirika ya umma hayana bodi za wakurugenzi, vikao vya bodi haviitishwi kwa wakati, na baadhi ya mashirika hayo huchelewa kukamilisha hesabu zao za mwaka kwa wakati.

No comments:

Post a Comment