HOME

Apr 21, 2012

SPIKA WA BUNGE ABATILISHA ZOEZI LA KUKUSANYA SAHIHI ZA WABUNGE KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU!!

Mh. Anna Makinda spika wa bunge la Tanzania
Mh. Kabwe Zitto
Spika wa bunge la Tanzania Mh Anne Makinda ametoa ufafanuzi juu ya azimio la  mbunge wa kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe ya kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kutoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu kwa nia ya kuwawajibisha baadhi ya mawaziri wanaoshutumiwa kwa ubadhirifu na hawataki kujiuzulu kwa hiari yao.


Spika Makinda amesema kutokana na kanuni za bunge pamoja na katiba ya nchi suala hilo halitawezekana kutokana na kutokukidhi baadhi ya vigezo kikiwemo kigezo cha kuwasilisha azimio ama hoja hiyo kabla ya siku 14 jambo ambalo haliwezekani katika mkutano huu wa saba.


Azma hiyo inafuatia taarifa zilizowasilishwa bungeni na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali pamoja na taarifa za wenyeviti wa kamati za tatu ambazo ni kamati ya mashirika ya umma (POAC),kamati ya serikali za mitaa (LAAC) na kamati hesabu za serikali kuu (PAC) ambapo mbunge wa Kigoma Kaskazini aliwaomba wabunge kuchukua hatua ya kuwawajibisha mawaziri ambao wanatajwa kwa ubadhirifu lakini hawataaki kujiuzulu wenyewe.


Mapema hii leo asubuhi zoezi la kukusanya saini 70 za wabunge bila ya kujali vyama wanavyotoka likaanza katika lango kuu la kuingilia bungeni likiratibiwa na mtoa hoja ambaye ni Mh. zito huku mbunge wa Ludewa Mh. deo Fililikunjombe akiwa ni miongoni mwa baaadhi ya wabunge waliotia saini na kueleza sababu za kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment