Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ameamrisha wanajeshi wake kuondoka kwenye visima vya Heglig katika mpaka unaozozaniwa kati yake na Jamuhuri ya Sudan.
Wanajeshi wa Sudan Kusini waliteka eneo la Heglig wiki jana ambapo walilaumu utawala wa Khartoum kutumia mahala hapo kama ngome ya kufanya mashambulio.
Siku ya Alhamisi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon alitaja kuwepo kwa wanajeshi wa Sudan Kusin kama kinyume na sheria ya kimataifa.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa ulitaka Jamuhuri ya Sudan kusimamisha mashambulio dhidi ya Sudan Kusini .
No comments:
Post a Comment