HOME

Apr 12, 2012

TRAORE AMEAPISHWA KUWA RAIS WA MPITO MALI!!

Rais Dioncounda Traore
Dioncounda Traore ameapishwa kuwa Rais wa mpito wa Mali kuashiria kurejea kwa utawala wa kiraia baada ya mapinduzi kutokea mwezi uliopita nchini humo.


Serikali ya spika huyo wa zamani sasa ina siku 40 za kuandaa uchaguzi ambapo waandishi wanasema muda huo huenda usitoshe kuandaa uchaguzi hasa kwa kuzingatia eneo la kaskazini kuwa mikononi mwa waasi.


Majukumu ya kiongozi wa mapinduzi Kepteni Amadou Sanogo hayajajulikana na Bw Traore aliapishwa na Rais wa mahakama Kuu Nouhoum Tapily katika hafla fupi mjini Bamako.


Mataifa ya Afrika Magharibi yaliondoa vikwazo vyake kwa Mali baada ya Kepten Sanogo kukubali kuachia madaraka.

No comments:

Post a Comment