HOME

Apr 5, 2012

AMINI AKANUSHA UVUMI KUWA ''AMEOA KIMYA KIMYA''!!

Moja ya picha zilizopo kwenye video mpya ya Amini.
Msanii wa muziki kutoka kundi la THT Amini Mwinyimkuu amekanusha uvumi unaosambaa katika mitandao pamoja na picha kuwa amefunga Ndoa Kimyakimya.


Amini amekanusha taarifa hizo akisema picha hizo ni sehemu ya video yake mpya anayotarajia kuitoa hivi karibuni inayokwenda kwa jina la ''Ni wewe'' ambayo anaifanya na kampuni ya Visual Lab chini ya Adam Juma.


Amesema hawezi kuzuia waandishi wa habari kufanya kazi yaio kuandika wanachotaka kuandika hata kama hawajathibitisha kutoka kwake na kuwataka mashabiki na watu wake wa karibu kusikiliza kutoka kwake kwani yeye ndio muhusika na sio mtu mwingine.

No comments:

Post a Comment