Mtuhumiwa wa mauaji ya watu wa 77 kwa shambulio la bomu na bunduki nchini Norway mwezi Julai mwaka jana Anders Behring Breivik amefikishwa mahakamani kwa mara ya pili leo ushahidi ukitolewa.
Mapema kesi hiyo iliahirishwa kwa muda baada ya jaji mmoja kuondolewa kutokana na matamshi aliyoyatoa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook mwezi Julai mwaka jana kuwa Breivik anatakiwa kukabiliana na adhabu ya kifo.
Breivik amesoma maelezo yaliyotayarishwa kwa muda wa dakika 30 na amekiri kuhusika na mlipuko wa bomu na kushambulia kambi ya vijana lakini amekana shitaka la ugaidi na mauaji.
No comments:
Post a Comment