HOME

Apr 4, 2012

MWANAMKE MZEE AWEZA KUIDHIBITI NDEGE BAADA YA MUME WAKE RUBANI KUZIMIA NA KUFA!!


Ndege iliyodhibitiwa na Bi. Collins isiweze kutua ghafla
 Mwanamke mzee raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 80 ambaye alikuwa na ufahamu kidogo wa kurusha ndege aliweza kuidhibiti ndege na kufanikiwa kutua kwa dharura huko Wisconsin baada ya mumewe rubani kuzimia na kufa.


Bibi huyo ambaye ametambulika kwa jina la Helen Collins alikuwa mtulivu wakati akishusha ndege hiyo ndogo aina ya Cessna na kutua katika uwanja wa ndege wa Cherryland pamoja na kwamba alijua mume wake amefariki.


Mwanae James Collins ambaye naye ni rubani aliyefuzu alimuongoza mama yake kwa njia ya radio na kufanikiwa kutua amesema mama yake aliwahi kufanya masomo ya msingi ya urubani ya kuruka na kutua miaka 30 iliyopita.

No comments:

Post a Comment