HOME

Apr 11, 2012

UCHUNGUZI AJALI YA NDEGE YA ATCL WAANZA!!

Uchunguzi wa ajali ya ndege ya shirika la ndege nchini Tanzania (ATCL) umeanza jana  mjini Kigoma ambapo timu ya watalaam watano wa mambo ya uchunguzi wa ajali za ndege watahusika na uchunguzi wa ajali ya ndege hiyo.

Rubani Mkuu wa ATCL kapten Richard Shahidi amewathibitishia  waandishi wa habari mjini Kigoma kuwa uchunguzi ulianza mara baada ya wao kuwasili.

Pamoja na kiongozi huyo pia timu hiyo itawahusisha Mkaguzi mkuu wa ajali za ndege kutoka ATCL, Method Barabara na Mhandisi Sahari Richard kutoka shirika hilo ambapo Sambamba na hao pia yupo John Nyamwira, Mkaguzi mkuu wa ajali za ndege kutoka wizara ya uchukuzi na msaidizi wake Lius Paul.

 Amesema ni mapema mno kusema chochote kwa sasa kuhusiana na ajali hiyo kwani baada ya
ajali watakabidhi ripoti ya uchunguzi serikalini. lakini alibainisha kuwa tayari kisanduku cha kurekodi mienendo ya safari za ndege kimeshapatikana na uchunguzi wao utaanzia hapo.

No comments:

Post a Comment