HOME

Apr 24, 2012

MVUA ZIMESABABISHA MAAFA NCHINI KENYA!!

Mvua zilizoanza kunyesha nchini Kenya zimeendelea kusababisha maafa ya vifo na uharibifu wa mali kwa wananchi huku kitengo cha mamlaka ya hali ya hewa nchini humo kikionya uwezekano wa kutokea mafuriko zaidi.

Wananchi wa Kenya wameshauriwa kutoa tahadhari kwa mamlaka husika wakati kukiwa na tishio la mafuriko katika maeneo ya jirani wakati mvua kubwa zikiwa zinaendelea kunyesha nchini humo.

Siku ya Jumatatu miili ya watu sita ilipatikana kutoka hifadhi ya taifa ya Hell's Gate huko Naivasha ambako waumini saba vijana waliokuwa wakifanya ziara kusombwa na maji siku ya Jumapili.

Maeneo yaliyotambuliwa na mamlaka ya hali ya hewa kukumbwa na mafuriko ni pamoja na Budalangi,Nyando, Elgeyo Marakwet, Baringo, Nairobi na mikoa ya Murang’a.

No comments:

Post a Comment