Kuongezeka ghafla kwa idadi ya vifo nchini Syria kumeibua mashaka juu ya uwezekano wa kufanikisha mpango wa amani wa umoja wa mataifa wa kusitisha mapigano.
Wanaharakati wamesema watu 70 waliuwawa jana wengi katika maeneo ambayo yamekuwa yakishambuliwa na majeshi ya serikali katika mji wa Hama.
Serikali ya Marekani imesema timu ya uangalizi ya umoja wa mataifa iliyoko nchini Syria iko katika hatari kubwa ambapo umoja wa mataifa unasukuma kuongeza idadi ya waangaliaji,na mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa Kofi Annan anatarajiwa kulipa taarifa baraza la usalama la umoja wa mataifa leo.
No comments:
Post a Comment