HOME

Apr 11, 2012

KAMANDA WA POLISI MKOA WA KINONDONI AKANUSHA TAARIFA ZA WATU KUFA KUTOKANA NA MSONGAMANO MAZISHI YA KANUMBA!!

Marehemu Steven Kanumba enzi za uahi wake
Msongamano wa watu Leaders siku ya mazishi
Kamanda wa polisi katika mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela ametoa kauli ya mwisho baada ya taarifa kuenea wakati wa msiba wa Kanumba kupitia sms, facebook & twitter kwamba kuna watu wamepoteza maisha baada ya kuzimia kwenye msiba huo.

Kamanda Kenyela amesema huo ni uvumi tu baada ya watu kuona watu wengi wakidondoka, sasa kwa imani zao wakadhani kwamba wamefariki lakini ukweli ni kwamba wengi walipewa msaada hapohapo na watu wa msalaba mwekundu na wengine walipata nafuu wakiwa njiani kupelekwa hospitali.

Amesema mpaka sasa hakuna taarifa yeyote ya mtu kufariki au kupata matatizo yoyote hata ya kuibiwa japo watu walikua wengi zaidi ya mategemeo na kwa umati huo pengine ulikua unafaa kutengewa eneo kubwa labda uwanja wa taifa, ndio maana ule msongamano ulichangia watu kuzimia kwa kupata mshituko na hata joto lenyewe lilichangia sana.

No comments:

Post a Comment