HOME

Apr 24, 2012

CUF YATOA MSIMAMO SAKATA TANDAHIMBA!!

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchu – CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
MSIMAMO WA CHAMA


-Serikali haitakwepa kuwajibika kwa hasara zilizojitokeza na watu walioumizwa katika tukio hilo.


-Serikali iwalipe wafanyabiashara wote kwa mali walizopoteza na majengo yaliyoharibiwa.


-Serikali iwalipe fidia watu wote walioumizwa kwa risasi au vipigo vya polisi katika operesheni hiyo ya kikatili ya polisi dhidi ya wananchi.


-Serikali iwafute kazi na iwafikishe mahakamani viongozi wote wa polisi na askari waliohusika na matukio hayo.


-Serikali imfukuze kazi mkuu wa wilaya ya Tandahimba ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa kushindwa kuongoza na kuwaeleza wananchi wa Tandahimba namna serikali inavyoshughulikia tatizo la malipo yao ya pili ya korosho.


-Vitendo walivyofanya polisi Tandahimba vinajenga uhasama mkubwa kati ya raia na jeshi la polisi. Serikali iunde tume huru maalum ya uchunguzi na ambayo haitawahusisha polisi ili ikafanye uchunguzi wa kina na wa wazi na kisha tume hiyo itangaze hadharani mambo iliyoyabaini na kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuondoa uwezekano wa vitendo hivyo vya kimakusudi na kikatili kujirudia mahali pengine ndani ya Tanzania.


-Tume ya Haki za binadamu ifanye uchunguzi wake kubaini uvunjifu wa haki za binadamu Tandahimba na kuwawajibisha wahusika na kupendekeza hatua za kuchukua hali hiyo isirudiwe Tandahimba na kokote Tanzania.


-Asasi za kiraia za haki za binadam na Msaada wa Kisheria wawape msaada wa kisheria wahanga na waathirika wa Tandahimba waweze kudai haki zao.


-Wakulima wapewe haki na uhuru wa kiuchumi wa kuuza korosho zao na mazao mengine kwa yeyote atakayewapa bei nzuri. Serikali iweke mazingira ya wafanya biashara kushindana kwa kuwapa bei nzuri wakulima  wa korosho na mazao mengine.

No comments:

Post a Comment