HOME

Apr 12, 2012

SYRIA IMEANZA KUTEKELEZA MAKUBALIANO YA KUSITISHA MAPIGANO!!

Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa Koffi Annan
Hali ya kusitisha mapigano imeanza kutekelezwa nchini Syria licha ya kuwa nchi za Magharibi zinatilia shaka nia ya serikali kutekeleza mapatano hayo.


Waandishi wa habari wanasema inaelekea kuwa pande zote zimesitisha harakati zao hakuna ripoti za maafa au vifo hadi sasa.


Hata hivyo kulikuwa na taarifa kadhaa za kufyatuliwa mizinga na risasi mapema asubuhi na vikosi vya kijeshi bado vipo mitaani.


Serikali ya Syria pamoja na vikundi vya wapiganaji wa upinzani wanasema watatekeleza mapatano hayo ya kusitisha mapigano,lakini watajibu mapigo iwapo wakishambuliwa..

No comments:

Post a Comment