Moto ulioibuka katika nyumba moja iliyoko mtaa wa Majengo katikati ya jiji la Arusha umeteketeza maduka nane,hoteli na baa na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
Moto huo ambao chanzo chake halisi hakijajulikana unaodaiwa kuanzia kwenye moja ya maduka yaliyoko kwenye nyumba hiyo pamoja na kubainika mapema ulisambaa kwa kasi kubwa licha yakuwepo kwa jitihada za kuudhibiti kutoka kwa wananchi na kikosi cha zima moto cha Manispaa ya Arusha.
Hata hivyo jithada hizo hazikuweza kuzaa matunda kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo ya vitendea kazi na gari la zima moto kuishiwa maji hadi vikosi vingine vilipofika ika eneo hilo kutoa msaada kikiwemo kikosi cha Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru na kikosi binafsi cha Night Support cha jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment