Bodi ya Benki ya Dunia imemchagua mwanazuoni wa Marekani, Jim Yong Kim kuwa rais wa Benki hiyo.
Rais huyo mpya wa benki ya dunia amesema mitaji ya soko kwa ukuaji wa uchumi ndio mfumo ambao unatakiwa kupewa kipaumbele kwa kila nchi.
Katika mahojiano yake na shirika la utangazaji la Uingereza BBC Dr. Kim amesema kuwa mfumo huo ni bora kwa kutengeneza ajira kuwakwamua watu kutoka kwenye umaskini.
Dr. Kim alichaguliwa kuwa rais wa benki kuu ya dunia siku ya Jumatatu na ndiye aliyekuwa chaguo la Marekani ingawa wadadisi wengi wanahoji uwezo wake na kuongeza kuwa kuteuliwa kwake kulitokana na utashi wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment