HOME

Apr 5, 2012

MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA YAMVUA UBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI BW. GODBLESS LEMA!!

Hali ilivyo sasa Arusha mjini baada ya hukumu hiyo kutolewa.
Mahakama kuu kanda ya Arusha leo imemvua ubunge wa jimbo la Arusha mjini Bw. Godbless Lema.


Mamia ya wakazi wa jiji la Arusha na maeneo ya jirani leo wamejitokeza katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katika kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo.


Jaji Gabriel Rwakibarila ametoa hukumu juu ya madai walalamikaji hao kwamba Lema alitoa kauli za udhalalishaji, matusi na kashfa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge wa CCM Arusha Mjini, Dk Batilda Buriani.


Akizungumzia hukumu hiyo Lema amesema anaamini hukumu hiyo imetolewa kisiasa na mchana huu anakutana na viongozi wake kitaifa katika ofisi za Chadema mkoa na baadae wananchi ili kujadili na kutoa tamko iwapo watakata rufaa ama laa.

No comments:

Post a Comment