HOME

Apr 26, 2012

WAZIRI AKIRI KUNUNUA NYUMBA YA MAMILIONI!!

Siku chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti taarifa za uchunguzi kwamba kuna mawaziri wawili ambao wamenunua nyumba mbili zenye thamani ya Sh1.8 bilioni, mmoja wa mawaziri hao, Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii ameibuka na kukiri.Maige aliliambia gazeti hili jana kuwa nyumba yake hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, ameinunua kwa Dola za Marekani 410,000 (takriban Sh656 milioni) ambazo anadai kuwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Hata hivyo, wakati Waziri Maige akieleza kuwa nyumba hiyo ina thamani hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amedai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba ilinunuliwa kwa fedha taslimu Dola 700,000 za Marekani (takriban Sh1.1 bilioni).

Awali, habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa Waziri Maige alinunua nyumba hiyo kutoka kwa Kampuni ya Savana Real Estate.

Mmoja wa madalali wanaouza nyumba za kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman (Ustadhi) alilithibitishia gazeti hili kwamba Waziri Maige amenunua nyumba moja kati ya nne zilizoko sokoni.
Habari na Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi zaidi INGIA HUMU.

No comments:

Post a Comment